MTIBWA SUGAR WAAMBULIA KICHAPO,POLISI WAPETA

HAMSINI Malale, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa anashukuru kwa ushindi aliopata mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa ligi.

Kwa upande wa kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma amesema kuwa sababu ya kushindwa kupata matokeo ni uwanja.

Ilikuwa ni mabao ya Datius Peter dk ya 43 kwa mkwaju wa penalti na Tariq Simba dk ya 84 yalitosha kuipa pointi tatu muhimu Polisi Tanzania mbele ya Mtibwa Sugar.

Unakuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Mtibwa Sugar kupoteza huku Polisi Tanzania ikpata ushindi baada ya kucheza mechi 7 bila kuambulia ushindi.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Ushirika Moshi na Polisi Tanzania waliweza kusepa na pointi tatu zote mazima.

Pia mchezo mwingine uliochezwa jana, Mei 25, Mbeya Kwanza iliweza kuichapa mabao 2-0 Kagera Sugar.

Ilikuwa ni kupitia mabao ya Eliuter Mpepo dk ya 51 na Jimmy Shoji dk ya 58.

Polisi Tanzania inafikisha pointi 30 nafasi ya 11 huku Mtibwa Sugar ikibaki na pointi 28 nafasi ya 12 na Mbeya Kwanza wao wapo nafasi ya 15 na pointi 24 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 7 na pointi 33