CHAMA HATIHATI KUWAKOSA YANGA NUSU FAINALI

 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama kuna hatihati kuweza kuukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

Mchezo huo ambao ni wa hatua ya nusu fainali unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mei 28,2022.

Mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kutinga hatua ya fainali ambapo atacheza na mchezo wa fainali na mshindi wa mchezo Coastal Union v Azam FC.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa mchezaji huyo amekuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

“Hatujawa na Chama kwenye mechi za hivi karibuni kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha hivyo akiwa sawa tutajua kama ataanza ama la.

“Kikubwa ambacho tutakifanya ni kusubiri ripoti ya madaktari itakuwa inaeleza nini ili tuweze kujua hao tutafanya nini,”