ILIBIDI mataifa matatu yaungane kuifunga Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi,Uwanja wa CCM Kirumba na kutibua rekodi ya dk 450 ya timu hiyo kutoruhusu bao.
Ni pasi ya kiungo Shaban Ada ambaye huyu ni mzawa alitoa pasi kwa Ambrose Awio raia wa Uganda kisha akampa pasi Collins Opare raia wa Ghana aliyeweza kufunga bao hilo dk ya 77 na kusawazisha bao lililofungwa na Fiston Mayele dk ya 74.
Yanga ilikuwa haijaruhusu bao tangu Aprili 23,2022 ilipocheza na Namungo Uwanja wa Mkapa iliposhinda mabao 2-1 na mtupiaji alikuwa ni mzawa Shiza Kichuya alitumia pasi ya Lukas Kikoti.
Katika mechi tano mfululizo, Yanga ilicheza ila kuruhusu bao ndani ya dk 450 rekodi ambayo ilitubuliwa na mastaa wa Biashara United.
Mechi ambazo Yanga ilicheza mfululizo bila nyavu zake kuguswa baada ya Kichuya kuwafunga ilikuwa namna hii:-Yanga 4-0 Mbeya Kwanza,Dodoma Jiji 0-2 Yanga,Prisons 0-0 Yanga, Ruvu Shooting 0-0 Yanga na Yanga 0-0 Simba.