SIMBA KUTUMIA MBINU ZA CAF KUIKABILI YANGA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa watatumia uzoefu ambao wamepata kwenye mechi za kimataifa kuweza kuwakabili Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

  Yanga ilitangulia katika hatua ya robo fainali kwa ushindi mbele ya Geita Gold hivyo itakutana na Simba katika mchezo wa nusu fainali Mei 28,Uwanja wa CCM Kirumba.

 Pablo amesema kuwa lengo la kwanza ilikuwa ni kuweza kutinga hatua ya nusu fainali kisha ushindi utafuata.

 “Tumecheza mechi ngumu na zenye ushindani mkubwa katika mashindano ya kimataifa, (Caf) hivyo uzoefo wa mechi hizo kubwa utatufanya tuweze kupata matokeo kwenye mchezo ujao.

 “Kitu kizuri ni kwamba tumeshinda na tunakwenda mbele katika mashindano haya, tutakutana na Yanga katika mchezo wetu wa nusu fainali hilo lipo wazi hivyo ninajua kwamba tutapata muda wa kufanya maandalizi,”.

 Zimebaki siku mbili kabla ya watani hawa jadi kuweza kukutana katika msako wa ushindi wa timu itakayokwenda hatua ya fainali.