KABLA ya mchezo kuanza Uwanja wa CCM Kirumba, George Mpole mshambuliaji wa Geita Gold na Kocha Mkuu, Felix Minziro wamekabidhiwa tuzo zao za mwezi Aprili.
Minziro alichaguliwa kuwa kocha bora na Mpole mwenye maao 14 akiwa ni mchezaji bora wa mwezi uliopita.
Ubao kwa sasa unasoma Geita Gold 1- Simba ikiwa ni mapumziko kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wenye ushindani mkubwa.
Kwa Geita Gold wao walianza kufunga dk ya 20 kupitia kwa George Mpole kisha Kibu Dennis aliweka usawa ilikuwa dk ya 27.
Mchezaji wa Simba, Shomari Kapombe amekwama kuyeyusha dk 90 baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa leo.
Na mpaka sasa ni kadi moja ya njano imetolewa kwa Joash Onyango wa Simba