PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mchezo wao wa leo dhidi ya Geita Gold utakuwa mgumu kutokana na aina ya wapinzani ambao wanakutana nao.
Simba wenye pointi 50 kibindoni wana kibarua cha kusaka pointi tatu nyingine leo mbele ya Geita Gold saa 10:00 jioni Uwanja wa CCM Kirumba huku Geita Gold nao wakiwa wanazihitaji pia.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-1 Geita Gold na mwamuzi wa kati alikuwa ni Martin Saanya.
Pablo amesema:”Utakuwa ni mchezo mgumu kwetu na hilo lipo wazi kwa kuwa Geita ina wachezaji wazuri na wanacheza kitimu hivyo tutawakabili kwa mipango makini,”
Jana kikosi hicho kikiwa na mastaa kama John Bocco, Meddie Kagere na Aishi Manula walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo.