YANGA YASEPA NA POINTI TATU MBELE YA MBEYA KWANZA

VINARA wa Ligi Kuu Bara leo wamesepa na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Mbeya Kwanza ya Mbeya.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha jumla ya pointi 63 ikiwa inazidi kuukaribia ubingwa wa ligi msimu wa 2021/22.

Ni mabao ya Fiston Mayele ambaye ametupia bao la kufungulia kwa Yanga dk ya 34 kisha msumari wa pili Said Ntibanzokiza alipachika bao dk ya 38, Dickon Ambundo amepachika bao dk ya 45 mbele ya Mbeya Kwanza.

Kipindi cha pili Mbeya Kwanza walikuwa na jitihada za kusaka mabao ila mikono ya kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui iliweza kuokoa hatari hizo.

Heritier Makambo ambaye alianzia benchi alipachika bao la 4 likiwa ni bao lake la kwanza msimu wa 2021/22 kwenye ligi ilikuwa dk ya 7