DODOMA JIJI WAJA NA HESABU KALI KWELI

BAADA ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Yanga,mpango namba moja kwa Dodoma Jiji ni kuweza kushinda mechi zao ambazo zimebaki.

Ikiwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma ilikubali kushuhudia mabao ya Dickosn Ambundo pamoja na la kipa wao Mohamed kujifunga jambo lililofanya wakapoteza pointi tatu mazima.

 Msemaji wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema wanamikakati mikubwa ya kuhakikisha wanashinda mechi zao zilizobaki kwenye ligi kuu.

  Msemaji wa Dodoma Jiji, Mpunga amesema: “Kufungwa au kupoteza kwa mechi hii sio sababu ya kuondoka malengo yetu kikubwa tunataka ushindi kwenye mechi zilizobakia.

“Bado tuna mechi sita, tatu ugenini na tatu nyumbani naamini inatutosha kumaliza ligi tukiwa nafasi ya nne.”

Dodoma Jiji iko nafasi ya 11 na ikiwa imecheza michezo 24 na kukusanya pointi 28 kwenye msimamo wa ligi kuu