SIMBA YABAKISHA DAKIKA 90 KUKUTANA NA YANGA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba kwa sasa ana dakika 90 za kuweza kuamua kama ataweza kukutana na Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Baada ya kukamilisha kete yake mbele ya Kagera Sugar,Mei 11 na kushinda mabao 2-0 sasa kituo kinachofuata ni mbele ya Pamba mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Ikiwa Simba itashinda basi itakuwa mikononi mwa Yanga iliyotangulia mapema kwa ushindi wa penalti 7-6 mbele ya Geita Gold uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dk 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Pablo amesema kuwa kila mechi kwao ni muhimu kupata ushindi ili kuweza kufikia malengo.

“Tunajua kwamba tuna mechi nyingi za kucheza na muhimu kwetu kushinda hivyo tutajitahidi kushinda mechi zetu zote ambazo tutacheza,”.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa leo Mei 14, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.