SIMBA:TUNALITAKA KOMBE LETU

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba unahitaji kuteteta taji la Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwao hivyo watapambana kupata matokeo.

Kesho, Mei 14 Simba ina kazi ya kusaka ushindi mbee ya Pamba katika mchezo wa hatua ya robo fainali unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ahmed Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji kombe lao.

“Tunajua kwamba kila mmoja analitazama hili kombe kutokana na umuhimu wa kuweza kuwa nalo na ni kombe ambalo lipo mikononi mwetu hivyo tutafanya vizuri kulitetea.

“Tunakutana na Pamba moja ya timu zenye uzoefu na wachezaji wazuri hasa ukizingatia kwamba ipo kwenye hatua hii ina maana ni wapinzani wazuri lakini hatuwabezi sisi tunahitaji kombe.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kuona namna tutakavyofanya Uwanja wa Mkapa na watafurahi wenyewe,”.

Ikiwa Simba itashinda kwenye mchezo huu hatua inayofuata ya nusu fainali itakutana na Yanga iliyotangulia katika hatua hii mapema kwa ushindi mbele ya Geita Gold.