NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanaga amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons wanaamini kwamba watashinda.
Leo Mei 9, vinara hao wa ligi wanatarajia kusaka pointi tatu mbele ya Prisons ambao nao wanahitaji pointi hizo, Uwanja wa Mkapa.
Maandalizi ya mwisho ameweka wazi kwamba yamekamilika na miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye orodha ya nyota waliokuwa wakifanya mazoezi ni pamoja na kiungo Farid Mussa.
Nabi amesema:”Tunatambua kwamba mchezo wetu dhidi ya Prisons utakuwa ni mgumu na ushindani mkubwa lakini tutapambana kuweza kushinda.
“Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anatambua kwamba ni muhimu kupata pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Prisons 1-2 Yanga.