WAKATI leo kikosi cha Tanzania Prisons ikiwa na kazi ya kuikabili Yanga,safu yake ya ushambuliaji inaonekana kuwa pasua kichwa kwenye utupiaji.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 22 ni mabao 15 imeweza kufunga ndani ya ligi katika dakika 1,980 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dk 132.
Kinara wa utupiaji wa mabao kwa Prisons ni Jeremia Juma mwenye mabao 5 akiwa ni staa wa kwanza kufunga hat trick msimu huu alipowatungua Namungo FC.
Wanakutana na safu namba moja kwa utupiaji Bongo, Yanga yenye mabao 35 baada ya kucheza mechi 22.
Yanga ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dk 56 na kinara wa utupiaji ni Fiston Mayele mwenye mabao 12.