LIGI inazidi kupamba moto kwa sasa na hilo lipo wazi hasa ukitazama namna ambavyo timu zinacheza kwa sasa kwenye mzunguko huu wa pili.
Ukitazama namna pointi walizoachana kuanzia yule aliyepo nafasi ya mwisho mpaka iliyopo ndani ya 10 bora sio namba ya kutisha na zote kwa sasa bado zinapambania kushuka daraja.
Ajabu ni kwamba hata zile ambazo zipo ndani ya tano bora kuna uwezekano wa kuweza kushuka daraja ikiwa zitakuwa kwenye mwendo mbovu wakati huu.
Kila timu inapata matokeo ambayo yanashangaza jambo ambalo ni gumu kwa kila mmoja kuamini kile ambacho anakiona.
Ugumu huu wa ligi uweze kuwa na matokeo mazuri kwa wachezaji kwani ni muda wa kukamilisha zile hesabu ambazo zipo kwa timu.
Hakuna namna ambayo unaweza kukwepa kushuka daraja lakini ipo namna ya kuweza kupata matokeo mazuri kwa kucheza vizuri.
Ikiwa utashindwa kupata matokeo kwenye mechi za lala salama nafasi ya kuweza kushuka daraja ipo mlangoni na hakuna ambaye anaweza kuwa salama.
Ikawe ni ushindani wa kweli kwenye mechi hizi ili kupata matokeo mazuri bila kutumia mbinu chafu kwenye kusaka ushindi.
Tunahitaji kuona mshindi anapatikana ndani ya uwanja baada ya dakika 90 kwa ukamilifu bila makele yoyote huku waamuzi nao wakitenda haki kwa kufuata sheria 17 za soka.