LICHA ya kuweza kuongoza mpaka dakika ya 87,Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Felix Minziro imekwama kusepa na pointi tatu mazima.
Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ambao ni wa ligi umechezwa leo Aprili 29,2022 Uwanja wa Nyankumbu.
Ni mabao ya George Mpole dk ya 26 na anafikisha bao la 11 ndani ya ligi na bao la pili kwa Geita Gold lilifungwa na Danny Lyanga ilikuwa dk ya 88.
Kwa Azam FC ilikuwa ni kupitia kwa Ismail Kader dk ya 35 na bao la kujifunga kwa beki Chilo Mkama ilikuwa dk ya 89.
Ilikuwa ni kwenye harakati za kuokoa hatari iliyokuwa inakwenda lagoni mwa timu yake hakuwa na namna katika kuokoa ikazama nyavuni mazima.
Sasa Geita Gold inafikisha pointi 28 ikiwa nafasi ya 6 na Azam FC ina pointi 29 ikiwa nafasi ya 4 zote zimecheza mechi 20.
Agrey Morris nahodha wa Azam FC amesema kuwa hali ya hewa ya mvua imetibua malengo yao ya kuweza kupata pointi tatu.