PRICE DUBE NI WA MWISHO KUIFUNGA YANGA

NYOTA Prince Dube mshambuliaji wa mwisho kuifunga Yanga na ikayeyusha pointi tatu mazima kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ilikuwa Uwanja wa Mkapa,Aprili 25,2021.

Leo Aprili 25, 2022 ni mwaka mmoja umemeguka tangu Dube kuitungua Yanga na msimu huu wa 2021/22 katupia bao 1.

Kwenye ligi,Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi imecheza jumla ya mechi 20 ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.

Inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza jumla ya mechi 20 ndani ya msimu wa 2021/22.

Mechi mbili walipokutana na Azam FC waliweza kushinda zote ambapo ule wa kwanza Uwanja wa Mkapa walishinda mabao 2-0 ule wa mzunguko wa pili walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Azam Complex.