YANGA YAITUNGUA NAMUNGO KWA MKAPA,MAYELE ATUPIA

BAADA ya dakika 90 kukamilika Uwanja wa Mkapa, kikosi cha Yanga kimeituliza Namungo FC kwa kuichapa mabao 2-1.

Ulikuwa ni mchezo mzuri wenye kasi ya ajabu mwanzo mwisho huku mikono ya makipa ikiwa kwenye harakati za kuokoa hatari zile za washambuliaji.

Fiston Mayele alifungua akaunti ya mabao Uwanja wa Mkapa ilikuwa dk ya 17 kisha nyota wa Namungo FC wakumuita Shiza Kichuya alifunga bonge moja ya bao akiwa nje ya 18 dk 33.

Wakati Namungo wakifikiria kuongeza bao la pili Yanga nao walikuwa wanafikiria hivyo na walimtungua David Kissu dk ya 39 kupitia kwa Feisal Salum.

Yanga wanaondoka na pointi tatu wakiwa Uwanja wa Mkapa huku Namungo wakiwa hawajaambulia pointi.

Yanga inafikisha pointi 54 ikiwa nafasi ya kwanza huku Namungo FC ikiwa na pointi 29 zote zimecheza mechi 20.