SIMBA YALIA NA MAPOKEZI YA ORLANDO PIRATES

MSAFARA wa viongozi pamoja na wachezaji wa Simba leo wamewasili salama nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Orlando Pirates ila wamebainisha kwamba mapokezi yalikuwa ni mabaya.

Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco ina kazi ya kusaka ushindi Aprili 24 kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya pili itakayoamua matokeo ya timu itakayotinga hatua ya nusu fainali, Kombe la Shirikisho Afrika.

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Simba wameachia ujumbe huu:”Asanteni Orlando Pirates kwa mapokezi mazuri lakini mmetunyima Polisi wa kutoongoza barabarani,(escorti) hivyo tumelazimika kutumia gari la Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kutuongoza,”.

Ni Meja Jenerali Gaudence Milanzi ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ameweza kuweka wazi kwamba kwa upande wa ulinzi na usalama ni wa kutosha hivyo wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa wasiwe na mashaka wacheze mpira.

Kwenye mchezo huo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ama sare ili kuweza kutinga hatua ya nusu fainali ubaya ni kwamba ikiwa itafungwa kwenye mchezo huo itafungashiwa virago mazima.