MASTAA SIMBA WAWAFUATA OLRANDO PIRATES

KLABU ya Soka ya Simba imeanza safari Alfajiri ya leo ijumaa 22, 2022 kuelekea nchini Afrika Kusini ambako itakwenda kucheza mechi yake ya marudiano dhidi ya Klabu ya Orlando Pirates ya nchini humo.

Simba inakwenda Afrika Kuisni ikiwa na faida ya ushindi wa bao moja ilioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 17 mwaka huu.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamekwea pipa ni pamoja na kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula,Shomari Kapombe, Jonas Mkude ambaye ni kiungo.

Pia Pape Sakho na Meddei Kagere ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wapo kwenye msafara huo.