TIMU sita zitashiriki katika mechi maalumu za kuadhimisha Wiki ya Wamachinga zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Karume.
Meneja wa Machinga wa Soko la Machinga Complex,Karume,Stellah Othman Mgumia alizitaja timu hizo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania,(TRA),Pepsi,Shirika la Bima la Taifa,(NIC),Mmalaka ya Chakula na Dawa, (TMDA) na Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo,(Taswa).
“Ni maandimisho ya kwanza ya wiki ya Machinga kwa Mkoa wa Dar na tumeanza kwa timu kushiriki katika michezo mbalimbali,”.
Miongoni mwa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Taswa ni pamoja na kiraka Wilbert Molandi.