SIMBA WAIVUTIA KASI ORLANDO PIRATES

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kimeanza kuwavutia kasi wapinzani kimataifa kwa ajili ya mchezo wao wa marudio.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi ama sare katika mchezo wao ujao dhidi ya Orlando Pirates baada ya ule wa awali ambao ni wa robo fainali ya kwanza kuweza kushinda bao 1-0.

Meneja wa Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa ambacho wanakifikiria kwa sasa ni nusu fainali.

“Kikosi kimeanza mazoezi ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wetu wa marudio dhidi ya Orlando Pirates nchi Afrika Kusini.

“Ambacho tunafikiria kwa sasa ni hatua ya nusu fainali hivyo maandalizi lazima yawe mazuri kuhsu siku ya kuondoka tutatoa taarifa lini tutaondoka,” amesema.

Alhamisi ya Aprili 21 kikosi hicho kinatarajiwa kuweza kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini.