SIMBA HESABU ZAO KUTINGA FAINALI ZIPO HIVI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa malengo makubwa ni kuweza kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika hivyo watahakikisha wanashinda hatua ya robo fainali ili kuweza kutinga hatua ya nusu fainali kisha fainali ili kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika.

Ofisa Habari wa Simba,Ahmed Ally amesema kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco na Seleman Matola, kocha msaidizi wao tayari wameingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wakiwa pamoja na wachezaji.

“Nguvu yetu na akili yetu,ni mchezo wetu dhidi ya Orlando Pirates na tunaiwaza robo fainali kuliko chochote kwa sababu tunahitaji kufanya vizuri katika mechi zote.

“Hakuna mwenye shughuli kubwa kwa sasa zaidi ya Simba hasa katika hatua ya robo fainali ambayo ni kubwa na itakuwa na matumizi ya VAR hivyo malengo yetu ni kuweza kuona watu elfu sitini wanakuwepo Uwanja wa Mkapa.

“Vikao mbalimbali vimekuwa vikiendelea kwa pande 4, Simba,TFF,CAF na Azam TV ili kuweza kuona kwamba kunakuwa hakuna changamoto yoyote katika matumizi ya VAR.

“Aprili 15 waamuzi watakosimamia VAR watafika Aprili 14 ni waamuzi ambao watasimamia mchezo watawasili nchini.
Kuhusu Orlando Pirates bado hawajatuambia siku watakayokuja kwa kuwa tunajua kwamba leo watakuwa na mchezo kisha wakituambia siku ambayo watakuja tutawaambia Watanzania ili waweze kwenda kuwapokea mashabiki wao.

“Tayari wachezaji wetu wamesharejea baada ya kupata kidogo mbele ya Polisi Tanzania ila mashabaki wasivunjike moyo kwa sababu tuna kila sababu ya kufanya kila namna tarehe 17 tunafanya maajabu makubwa.

“Malengo makubwa ni kuweza kuchukua ubingwa na tunapaswa Wanasimba kupigania ubingwa huu na tumesaliwa na mechi tatu ambazo ni tano kiujumla tukichanga karata yetu vizuri,tukichanga karata yetu vizuri tunakwenda kufanya vizuri kwa kuchukua ubingwa.

“Mtu timamu hawezi kuangalia kile kidogo ambacho amepoteza bali kikubwa ambacho kinakuja hivyo mashabiki na Watanzania tuweze kuungana katika hili, tayari tiketi zimeanza kuuzwa na tujenge utamaduni wa kununua tiketi mapema ili Jumapili iwe ni siku ya kuingia uwanjani.

“CAF wameturuhusu kuingiza mashabiki 60,000 ni Simba pekee ambayo imeweza kupewa ruhusa ya kuingiza full capacity ilikuwa ni kwenye mechi zote tulikuwa tunaomba turuhusiwe mashabiki elfu 60 na hii ni heshima kubwa kwetu.

“Ninaomba mashabaki waweze kujitokeza kwa wingi na kama tukiweza kuujaza uwanja basi itakuwa ni rahisi kwetu kuweza kupata nafasi ya kupata mashabiki wengi,tumecheza robo fainali mbili na zote tumetolewa lakini hii tumedhamaria.

“Orlando Pirates anapaswa kufia hapa na anapaswa kupigwa bao nyingi tu,shughuli hii haiwezi Aishi Manula pekee,Bernard Morrison pekee bali wote ikiwa ni pamoja na mashabiki lazima tuungane.

“Jumatano tutakuwa Kigamboni tutafanya balaa ndani ya pantoni,kama wewe ni shabiki wa timu nyingine majira ya saa 4 usipande pantoni na tutaanzia pale kwenye soko la Samaki, Alhamisi tunawatembelea wasomi Dar, Mlimani Campas tutazungumza nao na tutawaambia umuhimu wa wao kutenga siku moja kwa ajili ya Mnyama.

“Kila shabiki wa Simba anapaswa aje na skafu timu ikiwa inaingia tutakuwa tunapeperusha bendera huku tukiimba mnyama anafanya yake,ushangiliaji wa kipekee na safari hii tunainga wenzetu wa mbele huko.

“Tutaandaa tambara kubwa ambalo litauuzunguka uwanja mzima,sisi kama Simba hatubariki matumizi ya tochi,hatuzipendi hazitufurahishi kama klabu kwa sababu utamaduni huo haujawahi kutusaidia na utamuduni wetu ni uungwana,tunawaomba mashabiki wa Simba tuachane na hilo kwa kuwa tunaweza kupigwa faini.

“Tutakuwa na matumizi ya tochi za simu ambazo tutawasha wakati wa kuingia  ili tuweze kuupendezesha Uwanja wa Mkapa,” amesema Ally.