BAADA YA MAKONDA KUANDIKA UJUMBE MTANDAONI, MANARA AMUWASHIA MOTO

BAADA ya jana, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwajata anaodai wanataka kumuua, msemaji Yanga Haji Manara amemshukia Makonda.

Manara ameweka komenti kwenye posti ya makonda na kuandika hivi:

“Anaitwa Mungu, mkweli na kwa sasa hachelewi kujibu, leo unatafuta sympathy huku ukijua nn uliwafanyia watu?

Dhulma,dharau,kejeli,matusi na hata kuwaona Viongozi wenzio hawana maana,,ukawabambizia kesi za unga watu,,ukanyang’anya watu magari yao,

Sisahau siku uliyokataa kukaa jukwaani Pale Kwa Mkapa na kukaa ktk benchi kama Kocha kisa hutaki kusalimiana na mkubwa wako eti kisa hakupendi, Umesahau hata Mtoto wa mkubwa ukasema anauza unga na kutaka kumchafua kisa ulipata Cheo?

Acha kumsingizia Mungu,,waombe msamaha watanzania kwa dhulma zako,,na usitegemee Serikali ikuonee huruma, inajua everything about you, kina Sudi ukawasweka ndani bila sababu,,mm ndio nilikuwa mnyonge wako, hebu kwenda zako,,akuue Nani ww? Utajiua kwa stress zako mwenyew, cheo huna nenda kolomije kavue Sangara.” Mwsho wa nukuu!