AZAM V YANGA,ACHA INYESHE IJULIKANE PANAPOVUJA

MFUMO ni uleule wa kusaka ushindi kwa timu zitakazoshuka uwanjani na hii ya leo ni Dabi ya Dar es Salaam itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku.

Unaambiwa acha inyeshe tuone panapovuja baada ya dakika 90 itafahamika nani ni nani kati ya Azam FC v Yanga.

Timu zote zina wakali wa kucheka na nyavu na wale wakali wa kutupia cheki namna ilivyo;

WAKALI WA PASI NAMBA 4

Wakali wa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya vikosi vyote viwili ndani ya Azam FC na Yanga wametengeneza pasi 4 za mabao.

Ni Tepsi Evance wa Azam FC yeye alitoa pasi hizo ilikuwa mbele ya Geita Gold, Simba, Prisons na Dodoma Jiji mwendo wake ilikuwa ni mojamoja.

Kwa Yanga ni Saidi Ntibanzokiza yeye ametoa pasi nne alitoa pasi mbele ya Prisons, Mtibwa Sugar na alitoa pasi 2 mbele ya Kagera Sugar pia kiungo huyo ametupia mabao 6.

WAMEJENGA USHKAJI NA NYAVU

Rodgers Kola mwamba huyu ana ushikaji na nyavu akiwa na mabao matano kibindoni na pasi za mabao mbili hivyo amehusika kwenye mabao 7 kati ya 22 yaliyofungwa na Azam FC.

Ana rekodi ya kuwatungua watani wa jadi Simba walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Mayele ni mzee wa kutetema kwa Yanga akiwa ametupia mabao 10 na pasi 3 za mabao. Moja ya nyota ambao wamekuwa na kasi hasa wawapo karibu na lango.

Amehusika kwenye mabao 13 kati ya 31 ambayo yamefungwa na Yanga.

MABEKI WA KUPANDA NA KUSHUKA

Daniel Amoah huyu ni beki wa kupanda na kushuka popote anaonekana kwenye matukio muhimu. Kibindoni ametupia bao moja ilikuwa mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani.

Djuma Shaban huyu yeye kazi yake ni kumwaga maji akiwa ameweza kufanya hivyo mara mbili na katupia kibindoni mabao mawili.

WATAKOSEKANA

Iddi Chilunda, Keneth Muguna hawa walipata majeraha mazoezini hivyo ripoti ya daktari itaamua na Idd Nado huyu yupo nje kwa muda mrefu ni kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit.

Kwa Yanga ni kiungo Feisal Salum ambaye anatibu tatizo la misuli na Khalid Aucho huyu alipata maumivu akiwa na Timu ya Taifa ya Uganda.

@Dizo_Click.