MBEYA KWANZA WANA REKODI YAO BONGO

KIKOSI cha Mbeya Kwanza kinashikilia rekodi ya kuwa timu namba moja iliyoshinda mechi chache ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22.

Ikiwa imecheza mechi 18 ni mechi mbili pekee imeshinda ambazo ni dakika 180 huku ikiwa imeambulia kichapo kwenye mechi 8.

Sare imeambulia kwenye mechi 8 na kibindoni ina pointi 14 ikiwa nafasi ya 16 ambayo ni hatari kwa timu hiyo kuweza kushuka daraja ikiwa itaendelea kubaki hapo.

Safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao 14 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dk 115 ndani ya dk 1,620.