BAADA ya kutinga hatua ya robo fainali Simba imepangwa kukutana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco ina kibarua cha kuanza kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa, Aprili 17 mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kete ya mwisho itakayoamua Simba kutinga hatua ya nusu fainali itakuwa ni Aprili 24,Uwanja wa Orlando huko Afrika Kusini.
Droo imechezeshwa leo nchini Misri ambapo Simba itakutana na vinara wa kundi C waliomaliza wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 6.
Simba wao walimaliza wakiwa nafasi ya pili kundi D kibindoni walikusanya pointi 10 mchezo wao wa mwisho ulioamua matokeo ulichezwa Uwanja wa Mkapa
Wawakilisho hao kutoka Tanzania waliweza kufanya kweli dakika 45 za kipindi cha pili baada ya kuweza kufunga mabao 4 mbele ya USGN huku watupiaji wakiwa ni Sadio Kanoute aliyefunga bao moja huku Cris Mugalu akitupia mawili na bao moja kipa wa USGN katika harakati za kuokoa alijifunga.