KAGERA SUGAR WAGAWANA POINTI NA MTIBWA SUGAR

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar v Kagera umekamilika kwa timu zote mbili kutoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja.

Ubao wa Uwanja wa Manungu umesoma Mtibwa Sugar 1-1 Kagera Sugar hivyo hakuna mbabe ambaye amepatikana kwa vigogo hawa wawili.

Ni Mtibwa Sugar walianza kutupia dk 37 kupitia kwa George Chota ambaye alitumia pasi ya Said Ndemla.

Bao hilo lilidumu mpaka dk ya 69 ambapo Kagera Sugar walipachika bao kupitia kwa Erick Mwijage kwa pasi ya Mbaraka Yusuph.

Ulikuwa ni mchezo uliokuwa na ushindani kwa timu zte mbili ambapo Mtibwa Sugar waliweza kushindwa kulinda bao lao la kipindi cha kwanza walilopata.

Kila timu imefunga bao kwenye kipindi chake ambapo Mtibwa Sugar ni kipindi cga kwanza na Kagera Sugar ilikuwa ni kipindi cha pili.