KI AZIZ MIKONONI MWA MABOSI WA KARIAKOO

MSHAMBULIAJI wa ASEC Mimosas, Stephan Aziz KI anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa Kariakoo.

Nyota huyo amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu pamoja na kuwasumbua mebeki wa timu pinzani.

Ni ametupia mabao matatu katika Kombe la Shirikisho Simba na Yanga zinatajwa kuwania saini yake.

Nyota huyo aliwatungua Simba nje ndani walipokutana Dar na mchezo wa pili walipokutana nchini Benini katika mchezo wa kundi D ni raia wa Burkina Faso.

Simba inahitaji kuboresha safu ya ushambuliaji wake ili kuongeza nguvu kwa John Bocco na Meddie Kagere huku Yanga wakiwa na hesabu za kuongeza nguvu kwa Fiston Mayele.