WINGA JESUS MOLOKO ANAREJEA MDOGOMDOGO

WINGA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi emeanza kurejea mdogomdogo katika ubora wake.

Ni Jesus Moloko ambaye alikuwa chaguo la kwanza la Nabi kabla hajapata maumivu hivi karibuni.

Mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ilikuwa ni Februari 23,2022 na ubao ulisoma Yanga 0-0 Mbeya City ila kwa sasa taarifa zimeeleza kuwa anaendelea vizuri.

Kwenye msimamo Yanga ni namba moja ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 na haijapoteza mchezo hata mmoja ndani ya ligi.