UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa bado malengo yao ni kuweza kupata matokeo kwenye mechi zjazo licha ya kupoteza mbele ya Yanga.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa walipoteza mchezo wao uliopita kutokana na kushindwa kutumia nafasi hivyo makosa watayafanyia kazi.
“Tulikuwa na mechi muhimu dhidi ya Yanga na tulikuwa ugenini kwenye mchezo ule tulipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
“Kiuhalisia tulicheza vizuri na tulitengeneza nafasi kwa bahati mbaya hatukuweza kuzitumia na wenzetu waliweza kutumia makosa yetu.
“Ratiba sasa inaonyesha kwamba Aprili 3 tutakuwa na mchezo dhidi ya Namungo hivyo ni wakati wetu wa kujipanga kuelekea mchezo wetu dhidi ya Namungo.
“KMC siku zote tupo imara na hatuteteleki kwa ajili tulichokipata tupo nafasi ya 7 na katika duru ya pili tunataka kushinda mechi zilizobaki na tayari tumepoteza mechi mbili.
“Bado tuna nafasi kubwa ya kuweza kumaliza katika nafasi za juu ndani ya ligi,” amesema.