STRAIKA wa Azam FC, Prince Dube, amesema kwa sasa anahitaji kufunga mfululizo ili kuisaidia timu yake kumaliza ligi kwenye nafasi nzuri na kuwania Tuzo ya Ufungaji Bora msimu huu.
Dube aliyasema hayo baada ya kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu wakati Azam FC ikiibuka na ushindi wa mabao 1-2 dhidi ya Namungo kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi.
Wakati Dube akiwa na bao moja, kinara wa mabao Ligi Kuu Bara msimu huu ni Fiston Mayele wa Yanga mwenye kumi sawa na Reliants Lusajo wa Namungo.
amesema: “Namshukuru Mungu kwa kufunga bao langu la kwanza msimu huu, nafikiri huu ndiyo mwanzo wa safari yangu ya kufunga mfululizo ili kuisaidia timu yangu,”