UBAO wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 1-0 RS Berkane katika mchezo wa Kombe ma Shirikisho uliochezwa leo Machi 13.
Ni mchezo ambao ulimalizwa na Simba kipindi cha kwanza kwa bao pekee la ushindi la Pape Sakho dakika ya 44.
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa awali uliochezwa Morocco, Berkane ilishinda kwa mabao 2-0.
Florent Ibenge amekosa bahatu kushinda mbele ya Simba Uwanja wa Mkapa kwa kuwa hata alipokuwa akiinoa AS Vita aliwahi kufungwa.
Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya ASEC mchezo utakaochezwa nchini Ivory Coast.
Ushindi huo unaifanya Simba kuongoza kundi D ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi 4 kibindoni.