KIUNGO wa Simba, Clautos Chama raia wa Zambia amesema anawahusudu sana baadhi ya wachezaji wa kigeni kutoka kwa watani wao wa jadi Yanga.
Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Chama amesema pia anawakubali pia wachezaji wenzie wakigeni kwenye timu ya Simba.
“Nadhani nitawataja Pape Sakho, Peter Banda, Saido Ntibazonkiza, Aucho licha ya kuwa sijamtazama sana akiwa anacheza na Mayele naye anafanya vizuri tu.
“Mayele nimemuona kwenye mechi ambazo anacheza anafanya vizuri na inaonesha ni mchezaji mzuri hata kwetu pia wapo wachezaji wazuri,” amesema.
Ikumbukwe Chama amerejea tena Simba miezi kadhaa iliyopita akitokea klabu ya RS Berkane ya Morocco.
Kiungo huyo alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu uliopita na alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu wa 2020/21.