AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amesema kuwa wanaendelea vizuri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya RS Berkane.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili Machi 13 na mashabiki wamepewa nafasi ya kuweza kuuona mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Manula amesema kuwa wanatambua wapinzani wao watakuwa wanahitaji ushindi kwa kwa wao watakuwa nyumbani basi watapambana kupata ushindi.