IMEELEZWA kuwa Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inataka kumsajili mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Fiston Mayele (27) ili akawe mbadala wa mshambuliaji wao, Sebia Samir Nurković (29) ambaye huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu.
Mayele amekuwa na kiwango bora ndani ya kikosi cha Yanga ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao 10 na pasi za mwisho tatu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli ameandika ujumbe kuhusu tetesi hizo ambao unasomeka: “Basi leo simu zote za waandishi ni kuhusu Mayele kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Ninachoweza kuwahakikishia ni kwamba anakwenda Avic Town (Kigamboni).”