PRISON WATENGA MECHI ZA USHINDI

KOCHA Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba ameweka wazi kwamba mechi nne zijazo mbele zitawafanya warudi kwenye ubora wao.

Timu hiyo kwa sasa inatumia Uwanja wa Sokoine kama ilivyokuwa ikifanya zamani baada ya kuhamia Uwanja wa Nelson Mandela, Songea wakati walipokuwa kwenye maboresho ya kambi yao.

Prisons ipo kwenye mwendo wa kusuasa msimu wa 2021/22 ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 12 ni mechi 3 imeshinda,sare michezo 4 imepoteza michezo 10 baada ya kucheza mechi 17.

 Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Kazumba amesema kuwa mechi nne zinatosha kuwarudisha kwenye hali yao ya kawaida.

“Tutajitahidi kufanya vizuri kwenye mechi za ugenini kupambana na Biashara United na nyingine tatu za nyumbani ili tuweze kujitoa nafasi ya chini tuliyopo.

“Kwa upande wa timu ipo vizuri kwenye morali na kila mmoja anahitaji ushindi hivyo kutakana na hilo naamini Mwenyezi Mungu atatutangulia na kutuwezeshe kuwa nafasi nzuri.

“Mashabiki ni kama wachezaji wa kumi na mbili wakijitokeze kwa wingi kuja kushabikia timu yao nyumbani hata ugenini tunaamini mashabiki wanahamasisha wachezaji wakiwa uwanjani tunaomba wajitokeze kwa wingi uwanjani na sisi hatutawaangusha tumeanza na droo naimani ushindi utakuwepo mchezo unaokuja”.