Kama ilivyodesturi ya Meridianbet kurudisha kwenye jamii inayoizunguka, safari hii, kampuni ya Meridianbet Tanzania imetoa mkono wa pongezi kwa kina mama waliojifunga na wanaotarajia kujifungua kwenye Hospitali ya Mkoa Ya Rufaa, Mwananyamala.
Tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka, ni siku maalumu ya kumsherehekea mwanamke kote duniani. Siku hii ni mahsusi katika kumpatia thamani mwanamke ambaye, kwa miaka mingi, wanawake wamekua wakipitia changamoto mbalimbali kwenye jamii zetu bila kujali uwezo wao wa kufanya mambo makubwa na yenye tija kwa jamii inayowazunguka.
Katika kuchagiza na kumtambua mwanamke, Meridianbet Tanzania imeungana na watu wote duniani katika kusherehekea Siku ya Wanawake duniani ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wa wanawake na jamii kwa ujumla. Kwa upekee wa siku hii, Meridianbet wamewatembelea kina mama waliojifungua (pamoja na wale wanaotarajia kujifungua) katika Hospitali ya Mwananyamala.
Katika kuwatembelea huko, Meridianbet imetoa zawadi za pongezi kwa kina mama hao ikiwa ni pamoja na mahitaji muhimu kwa kina mama waliojifungua kama vile; kanga, sabuni na mafuta kwa ajili ya mama na mtoto. Vilevile, kampuni hiyo imetoa baadhi ya vitendea kazi kwa wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala waowahudumia kina mama ikiwa ni pamoja na vikinga mikono (gloves), jik n.k.
Akizungumza na kinamama hospitalini hapo, Afisa Masoko wa Meridianbet, Bwana Twaha Ibrahim ambaye pia aliambatana na wafanyakazi wengine wa Meridianbet – Bwana Baraka Kato na Bwana Amani Maeda, alisema “pongezi za dhati kwenu kinamama wote ambao kwa hakika, mnaisherehekea vyema siku hii ya wanawake duniani. Sisi Meridianbet, tunaungana pamoja nanyi katika kusherehekea uwezo wenu mkubwa wa uumbaji ambao ama hakika, mnakila sababu ya kujivunia uwezo wa kuongeza vijana wengine watakaokwenda kuendeleza gurudumu la maendeleo nchini. Pongezi nyingi kwenu wanawake na kina mama kwa ujumla”
Aidha, akipokea mkono wa pongezi kutoka Meridianbet, Katibu wa Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Rufaa, Mwananyamala – Bi. Lilian Mwanga, amewashukuru Meridianbet kupitia wawakilishi waliofika hospitalini hapo akisema, “kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya Mwananyamala, tunawashukuru sana (Meridianbet) kwa kuthamini na kuona umuhimu wa mwanamke ikiwa ni pamoja na kuona umuhimu wa kurudisha kwenye jamii. Tunawakaribisha tena kwenye hospitali yetu na kama mnavyofahamu, hii ni taasisi ya serikali na tunatoa huduma ya uzazi bure kwa kina mama na watoto ambapo pia, mahitaji yao ni mengi katika kuwahudumia. Tunashukuru sana kwa ujio wenu na tunaamini mtaendelea kututembelea na kusaidia kwa kadiri itakavyowezekana”
Meridianbet inaendelea kuwa bega kwa bega na jamii inayoihudumia ikiamini kuwa, mahusiano bora na wanajamii ni chachu ya maendeleo kwa Taifa. Hakika, hii ni familia ya kila mmoja anayeamini katika ubingwa. Kheri ya siku kuu ya wanawake duniani kutoka kwenye familia ya Meridianbet Tanzania!
Meridianbet – Bashiri Popote, Wakati Wowote.