RATIBA YA SIMBA MACHI NI BALAA

BAADA ya wawakilishi wa Tanzania kimataifa Simba kurejea salama Dar wakitokea Morocco wana vigongo vya moto ndani ya Machi kutimiza majukumu ya kusaka ushindi.

Ikumbukwe kwamba Februari 27 walinyooshwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa kundi D kituo kinachofuata ni dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kuchezwa Machi 4 Uwanja wa Mkapa kisha Machi 7 watamenyana na Dodoma Jiji, Uwanja wa Mkapa na watasepa mpaka Uwanja wa Ushirika Moshi kumenyana na Polisi Tanzania.

Itakuwa ni Machi 27 kwa mechi za ligi na RS Berkane watamenyana nao Machi 13 na ASEC Mimosas watakutana nao Machi 20 hizi ni za kimataifa.