AZAM FC YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA COASTAL UNION

JOHN Matambala, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa Coastal Union ilikuwa imara eneo la katikati huku akiwaomba mashabiki kuendelea kuwa wavumilivu.

Machi Mosi, ubao wa Uwanja wa Azam Complex umesoma Azam FC 0-0 Coastal Union na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

“Tumetoka kupoteza mechi,ninawapongeza Coastal Union kwa kuonyesha mchezo mzuri. Mashabiki wasikate tamaa,mpira upo hivyo duniani kote,”

Kwa upande wa Joseph Lazaro, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa hawakuhitaji kufunga ila pointi tu.

“Tulijua hali hii ingetokea tulikuja ili tupate pointi na tumefanikiwa, narudia tena hatukuja kufunga ila tulikuwa tunataka pointi moja ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji, “.