SHABIKI WA SIMBA,ARSENAL ASHINDA SH 176.5 M ZA M-BET

SHABIKI wa Klabu ya Simba na Arsenal Swalehe Enzi ameshinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

Enzi ambaye ni mkazi wa Mtwara ameshinda kiasi kikubwa cha fedha hizo baada ya kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za soka za ligi mbalimbali duniani kwa kutumia sh1,000 tu.

Alisema kuwa amebashiri kwa kipindi cha miaka mitatu huku akishinda kiasi cha fedha kidogokidogo ambazo hazikumkatisha tamaa.

Alisema kuwa pamoja na yeye kuwa shabiki wa Simba na Arsenal, bado huwa anakumbana na vipingamizi vingi katika kubashiri kwake jambo ambalo limekuwa likimharibia ‘mkeka’ wake na ‘kuchanika’.

“Mimi ni fundi seremala na nimekuwa nikibashiri kwa kutumia madaftari au ‘counterbook’. Nimefanya hivyo kwa miaka mitatu huku nikishinda zawadi za fedha ndogo ndogo.

“Sikuweza kukata tamaa kwani nimeshuhudia washindi kadhaa kupitia Perfect 12 ya M-BET wakishinda fedha mamilioni. Nilijua ipo siku nami nitashinda kwani hakuna ubabaishaji, natoa wito kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18, kubashiri kupitia M-BET,” amesema Enzi.

Alisema kuwa hakuamini kupigiwa simu kuwa ameshinda kiasi kikubwa cha fedha hicho na sasa kuwa na mipango ya kuendeleza biashara na kuanzisha nyingine, kusomesha na kujenga nyumba.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia mchezo yao.

Mushi alisema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakibashiri na kushinda kupitia michezo yao na kufanikiwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari washindi wamepatikana. Tutaendelea kuwa nyumba za washindi na kubadili maisha ya Watanzania,” alisema Mushi.