NYOTA DODOMA JIJI ALIYECHEZA YANGA AANZA KAZI

WAZIR Junior, ingizo jipya ndani ya kikosi cha Dodoma Jiji amefungua akaunit yake ya mabao kwa kutupia mbele ya Ruvu Shooting.

Tayari ameanza kazi ya kucheka na nyavu na kituo kinachofuata ni mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 5.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Dodoma Jiji ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na ilikuwa inanolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata ambaye kwa sasa amefutwa kazi na nafasi yake ipo kwa Masoud Djuma.

Jr alifanya hivyo Februari 27 Uwanja wa Mabatini walipokuwa wakicheza na Ruvu Shooting na mchezo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 hivyo timu hizo ziligawana pointi mojamoja.

Ulikuwa ni mchezo wa kwanza kutupia kwake baada ya kujiunga na Dodoma Jiji baada ya kujiunga na timu hiyo akiwa ni mchezaji huru.

Mshambuliaji huyo alivunja mkataba na timu yake ya Yanga ambayo ilimsajili katika dirisha kubwa akitokea Klabu ya Mbao FC.