KIKOSI cha Yanga kimesepa na pointi tatu mbele ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni mabao matatu ambayo yamefungwa kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Fiston Mayele ametupia mabao mawili na pasi moja ya bao, amefunga dk 30 na 50 pasi kampa mshikaji wake Said Ntibanzokiza dk ya 64.
Yanga inafikisha pointi 42 ikizidi kujikita nafasi ya kwanza kwa msimu wa 2021/22.
Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata jambo lililofanya wakapoteza.
“Tulitengeneza nafasi kwenye mchezo wetu na ilikuwa ni mchezo mzuri ila mwisho wa siku tumepoteza hivyo tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo,”.