UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba unahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kwamba wanahitaji kupata pointi tatu mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa mchezo ni mgumu na wanaamini watapata ushindi.
“Mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar utakuwa mgumu lakini tunahitaji kupata pointi tatu na jambo la msingi ni kuona kwamba tunashinda na kupata pointi tatu.
“Kwenye mchezo wetu wa mzunguko wa kwanza tulipata matokeo hivyo tunahitaji kushinda tena kwa mchezo wetu huu wa mzunguko wa pili na tunaanza palepale ambapo tuliishia,” amesema Bumbuli.
Kwenye mchezo wa kwanza, Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-0 Kagera Sugar, mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum.
Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 39 imetupia mabao 25 kinara wa kutupia mabao akiwa ni Fiston Mayele ambaye ametupia mabao 7 na pasi mbili za mabao.