SIMBA:TUTASHINDA MBELE YA RS BERKANE,WATANZANIA MTUOMBEE

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari wa ajili ya mchezo wao dhidi ya RS Berkane ya Morocco unaoatarajiwa kuchezwa Jumapili na wanaamini kwamba watashinda.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco, Februari 27 inakibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa hatua ya makundi wakiwa katika kundi D.

Barbara amesema:”Tumetoka kupata pointi moja kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya USGN ya Niger ulikuwa ni mchezo mgumu lakini tumepata pointi hilo tunamshukuru Mungu.

“Wachezaji wapo tayari kikubwa watuombee dua unajua timu yetu ni nzuri na kubwa, naomba watuombee sana ili tuweze kupata pointi na Jumatatu tunaamini tutakuwa tunaongea mambo mazuri zaidi,”.

Baada ya Simba kumalizana na USGN ya Niger waliibukia Uturuki kisha wakaunganisha safari mpaka Casablanca, Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.