VIDEO;YANGA WABAINISHA KUHUSU UBINGWA

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa kesho Februari 23, Uwanja wa Manungu wapo tayari na benchi la ufundi linahitaji ushindi.

Manara ameweka wazi kwamba Mtibwa Sugar ilishawahi kuwa bingwa wa ligi mara mbili mfululizo na uzoefu katika kushiriki mashindano makubwa na tangu imepanda ligi mfululizo wapo kwenye ligi huku akibainisha kwamba ukiacha Yanga na Simba hakuna timu ambayo imecheza kwa muda mrefu bila kushuka daraja.