NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuna presha kubwa katika kusaka ushindi uwanjani ambao utawapa ubingwa kutokana na kila timu kupiga hesabu za kuifunga Yanga.
Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 36 kibindoni baada ya kucheza mechi 14, ndani ya ligi hiyo
hawajapoteza mchezo msimu huu, huku Jumatano ijayo wakitarajiwa kupambana na Ruvu Shooting.
Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Presha inakuwa kubwa hasa timu inaposaka ushindi, ukizingatia kwamba ili uwe bingwa ni lazima ushinde mechi zako, hivyo hakuna tatizo katika hilo, tunalifanyia kazi.
“Kwa timu ambazo tunakutana nazo ninaona kwamba zinataka kuifunga Yanga, hapo inafanya kila mechi kwetu kuwa ngumu. Lakini inatakiwa kuwa hivyo kwa kuwa unapokuwa unashindana na mpinzani lazima awe ana malengo ya kushinda kama ambavyo sisi tunahitaji kushinda.”
Mchezo ujao wa Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar, Dickosn Job beki wa kati atakosekana kwa kuwa anaadhabu anatumikia.