SIMBA YAWAFUATA USGN YA NIGER

WAWAKILISHI wa Tanzania kimataifa katika Kombea Shirikisho, Simba leo wanatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Niger.

Simba itakuwa na mchezo dhidi ya USGN ya Niger ambao ni wa makundi katika Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa kwanza wa Simba katika Kombe la Shirikisho walishinda mabao 3-1 ilikuwa dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Ni Shomari Kapombe, Pape Sakho ambaye bao lake lilichaguliwa kuwa bao bora la wiki pamoja na Peter Banda walitupia katika mchezo huo.

Pia leo nyota hao ni miongoni mwa wale ambao wapo katika msafara wa wachezaji ambao wanaelekea Niger kwa ajili ya mchezo huo muhimu katika kundi D.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi hizo za kimataifa.