Ubora wa hali ya hewa umekuwa ukiongoza mijadala mikubwa ya masuala ya kimataifa kwa miongo kadhaa sasa. Ndio maana Meridian Gaming Group inafanyia kazi moja ya miradi mikubwa ya mazingira kwa sasa.
Kampuni hii inafanya kazi katika masoko zaidi ya 30 Ulaya, LATAM na Afrika, inapanga kutoa zaidi ya miche 20,000 katika kila soko inaloendesha shughuli zake ili kuongeza jitihada kwenye shughuli za upandaji kikamilifu.
Mradi huu, wenye lengo la kuboresha ubora wa hewa na afya ya umma duniani kote, tayari umeanza Ulaya, na utachukua sura ya kimataifa tangu kuanza kwake.
Mradi mkubwa wa mazingira pia utajumuisha mchango wa rasilimali muhimu za kifedha kwa serikali za mitaa kwa mahitaji ya mipango ya ardhi na kijiographia.
Hii ni sehemu ya ajenda kijani ya Meridian, ikiwa ni muendelezo wa jitihada za tangu 2020 ambapo maduka yake ya rejareja huko Ulaya yanatumia visafishaji hewa vya ubrora wa hali ya juu, vilivyoundwa kwa mujibu wa Maelekezo ya EU 125/2009 kuhusu ubora wa hali ya hewa Ulaya – CEN 14511.
Wakati huo huo, mchango wa kampuni hii katika kupambana na majanga umekuwa mkubwa hadi sasa. Zaidi ya euro milioni 2 kwa miradi na misaada inayohusiana na Covid zilitolewa kuisaidia jamii, na wakifanikiwa pia kuzifikia zaidi ya hospitali 350 na vituo vya matibabu vya Uropa, LATAM na Afrika kwa ujumla.
Kwa Tanzania, Meridianbet wameendelea kuwa kampuni nambari moja kwa ubora na masoko ya michezo ya kubashiri, kuanzia madukani hadi mtandaoni. Kampuni hii kongwe inaahidi kufanya vyema katika uwajibikaji kwa wateja wake kwa huduma bora, na kuendelea kurejesha kwa jamii.