MASTAA sita wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ikiwa ni pamoja na Sadio Kanoute, Pape Sakho leo Februari 16 wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora Uwanja wa Mkapa.
Kanoute na Sakho waliumia kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho na Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na Sakho alitupia bao moja pia.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji hao wanaendelea vizuri baada ya vipimo kueleza kwamba hawajapata maumivu makubwa.
Mbali na nyota hao wawili pia kiungo Taddeo Lwanga ,Chris Mugalu na Kibu Dennis hawa nao wanatarajia kuukosa mchezo wa leo kwa sababu bado hawajawa fiti.
Bernard Morrison ambaye amerejea kambini na kuanza mazoezi baada ya kusamehewa uwezekano wa kuanza leo ni mdogo huku maamuzi yakiwa mikononi mwa kocha Pablo.
Simba jana walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo na miongoni ambao walikuwepo mazoezini ni pamoja na Kanoute, Lwanga na Morrison.
Lwanga anakumbukwa kwamba ndiye aliyefunga bao la ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.