BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku Jumanne ya Februari 15 amesaini mkataba wa kupanda ulingoni kuzichapa dhidi ya Alex Kabangu kutoka DR Congo katika pambano litakalopigwa Machi 26, mwaka huu katika Ukumbi ambao utapangwa mkoani hapa.
Kiduku atapanda ulingoni kwenye pambano hilo la kimataifa baada ya kumchakaza Dullah Mbabe Agosti mwaka jana katika pambano lililopigwa kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Kiduku amesema kuwa amesaini kucheza pambano hilo dhidi ya Kabangu ambalo litachezwa Machi 26.
“Ni kweli nimesaini kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la mkanda wa ubingwa, naamini mkanda utabakia kwa sababu lazima nifanye maandalizi ya kutosha chini ya kocha wangu Pawa Ilanda.
“Kila kitu tayari kimeshapangwa na promota juu ya siku ya pambano lakini maombi yangu ni kuweza kuwezasha pambano kufanyika mjini ili watu wengi waweze kuhudhuria taofauti na Magadu kwa sababu ni mbali na mjini,”