HATIMAYE siku iliyosubiriwa kwa shauku kubwa na wapenda soka duniani hiyo leo hiyo Simba SC vs Yanga SC imewadia.
Wababe hawa wawili wanatarajiwa kutupa kete ya kusaka ushindi mzunguko wa kwanza saa 1:00 usiku, Uwanja wa Uhuru.
Simba SC wenyeji baada ya mechi 6 hawajapoteza mchezo kama ilivyo watani zao wa jadi Yanga SC. Kwenye eneo la ulinzi timu zote zimeruhusu kufungwa mabao 2 jambo linaoongeza ugumu kwa kila timu kusaka ushindi.
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo wa leo kila mmoja atapambana kutimiza majukumu ndani ya uwanja.
“Wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo na tunawaheshimu wapinzani, kikubwa ni utayari na kila mmoja kuingia kusaka ushindi,”.
Kocha Mkuu wa Simba SC, Manqoba Mngqithi amesema kuwa wanatambua ugumu wa mchezo wataingia kwa tahadhari kusaka pointi 3 muhimu.
“Tunatambua ugumu wa mchezo na ushindani uliopo. Tutaingia uwanjani kwa nidhamu na malengo ni kumiliki mchezo na kupata matokeo chanya,”.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.